Msafara wa mwenyekiti UVCCM wapata ajali - Mpekuzi Huru | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Msafara wa mwenyekiti UVCCM wapata ajali

Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James,  umepata ajali wilayani Meatu baada ya gari la polisi lililokuwa kwenye msafara huo kuchomoka tairi.  Hakuna taarifa ya kifo,  lakini majeruhi watatu wamekimbizwa katika hospitali ya Mwandoya.
Ajali hiyo imetokea katika mpaka wa wilaya za Meatu na Itilima katika kijiji cha Kisesa ambako wakuu wa wilaya hizo walifika na kutoa misaada iliyotakiwa mara moja.
Wakati huohuo, basi la Rombo liligonga gari la madiwani kwa nyuma katika tafrani iliyofuatia baada ya kuchomoka kwa tairi la gari la polisi. Madiwani waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni wa kata za Imalaseko, Mwasengera na Ngh’oboko.


Source: Mpekuzi HuruRead More