Msanii Barnaba Azimia Akimuaga Ruge (Picha) - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Msanii Barnaba Azimia Akimuaga Ruge (Picha)

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barnaba Boy ‘Classic’ amesababisha vilio Kutawala Baada ya kuzimia wakati akitoa hotuba fupi ya mazishi ya baba yake mlezi  Ruge Mutahaba.


Barnaba amesababisha vilio kutawala baada ya kushindwa kumalizia hotuba yake huku akiomba afunguliwe jeneza kumuona baba yake mlezi, Ruge Mutahaba.Msanii huyo kutoka THT aliondolewa ukumbini akiwa amebebwa baada ya kuishiwa nguvu kutokana na uchungu mkali alio nao.Kwenye hotuba yake Barnaba Alisema Ruge alikuwa kama baba kwake Baada ya kupoteza wazazi wake kwa kipindi kirefu Lakini pia Barnaba aligusia ugonjwa wa figo wa marehemu.Kama shida ni figo ungeniambi nikupe yangu, wazazi wangu walifariki Ruge ndio alikuwa Baba na ndio mama, Watoto wengi unawaoona THT wametoka kwenye maisha ya shida, Ruge alikuwa ndio Baba yetu” . 


The post Msanii Barnaba Azimia Akimuaga Ruge (Picha) appeared first on Ghafla! Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More