Msanii maarufu nchini Jamaica ‘Spice’ atukanwa mtandaoni kwa kujichubua, mwenyewe aeleza sababu ya kufanya hivyo - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Msanii maarufu nchini Jamaica ‘Spice’ atukanwa mtandaoni kwa kujichubua, mwenyewe aeleza sababu ya kufanya hivyo

Msanii maarufu nchini Jamaica, Spice amejikuta akiambulia maneno makali kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya kufuta picha zote za zamani na kuweka picha mpya zikimuonesha akiwa mweupe tofauti na asili yake.


Spice

 


Spice ambaye anatajwa kama Malkia wa muziki wa Dancehall nchini Jamaica, amesema sababu ya kufanya hivyo ni baada ya kuachana na menejimenti yake iliyokuwa ikimsimamia awali ambayo amekuwa akisumbuana nayo kuhusu kuachia Album.Hata hivyo, leo Spice ameachia Kanda Mseto (Mix Tape) yake mpya iitwayo CAPTURED, ambayo watu wengi wameeleza kuwa huenda ndio imepelekea mrembo huyo kufanya hivyo.


Spice miezi miwili iliyopita alikuwa barani Ulaya kwenye Ziara yake ya muziki aliyoifanya zaidi ya nchi 5 na zote alisepa na kijiji.


Moja ya nyimbo za Spice ambazo zilishawahi kufanya vizuri duniani kote ni wimbo wake wa Conjugal Visit na ule wa Needle Eye.The post Msanii maarufu nchini Jamaica ‘Spice’ atukanwa mtandaoni kwa kujichubua, mwenyewe aeleza sababu ya kufanya hivyo a... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More