Msanii Makamua Aanika Kuwa QJay Amekuwa Kichaa - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Msanii Makamua Aanika Kuwa QJay Amekuwa Kichaa

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Makamua ameweka wazi kuwa msanii mwenzake Q Jay aliyewahi kutamba na nyimbo kali kama vile ‘Sifai’ amepata kichaa.


Makamua amedai Msanii huyo ana hali mbaya na kichaa chake kiasi ya kwamba kwa hivi sasa anaokota makopo na hivyo amewaomba Watanzania wamsaidie.


Kwenye Interview aliyofanya na Bongo5 rafiki wa karibu na msanii huyo, Makamua amesema kuwa kwa sasa Q Jay yupo Bukoba na amekuwa kama chokaraa kwani amekuwa anaokota makopo na kuongea vitu visivyoeleweka.


Makamua ameweka wazi kuwa kilochosababisha mpaka Msanii huyo kupatwa na majanga ni matokeo ya kimaisha baada ya kuachana na Familia yake na ugumu wa kimaisha.


Makamua ameweka wazi kuwa wakati jitihada za kumsafirisha Bukoba kuja Dar Es salaam zinaendelea amewaomba Watanzania wamchangie pesa za matibabu kwani Madaktari wamemueleza kuwa anahitaji msaada wa ushauri na nasaha kutoka kwa watalaamu wa Saikolojia.


The post Msanii Makamua Aanika Kuwa QJay Amekuwa Kichaa appeared first on Ghafla!Tanzani... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More