MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE

Na Khadija Seif,Globu ya jamii
MSANII nguli nchini kwenye tasnia ya filamu ya maigizo Hashim Kambi ahimiza nidhamu iwe ni kipaumbele kwa wasanii wenye majina maarufu pamoja na chipukizi katika kukuza  tasnia hiyo.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia mienendo ya baadhi ya wasanii ambapo amesema hairidhishi na inasababisha wasanii kutopata nafasi kwenye masoko ya nje huku akitolea mfano nchi jirani kama ya Kenya.
Kambi amesema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya wasanii wa Tanzania na Kenya ambapo, wasanii wa nchi hiyo wanazingatia nidhamu kwa kiwango cha hali ya juu bila kujali ukubwa au udogo wa jina na wanaheshimiana katika kazi zao za sanaa.
Pia amesema wasanii wenye majina  huwapa kipaumbele wasanii wakongwe ambao ambao wapo kwenye tasnia kwa muda mrefu na kuona ni fursa adhim kwa wakongwe hao kuendelea kutoa mafunzo na ujuzi ili kuleta mapinduzi katika sekta ya  filamu nchini.
Kuhusu sanaa yake ya uigizaji wa filamu , Kambi amesema kwa sasa ameshiriki kwenye fi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More