Msanii Snura Mushi na Mpenzi Wake Wapata Ajali Ya Gari - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Msanii Snura Mushi na Mpenzi Wake Wapata Ajali Ya Gari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko ya Mduara Snura Mushi ‘Snu Sexy’ pamoja na mpenzi wake Minu Calypto wamepata ajali ya gari siku ya jana mkoani Lindi walipokuwa anaelekea Kwenye shoo.


Taarifa za awali zinadai kuwa ajali hiyo ilitokea wakati Dereva wa gari la Snura alipokuwa anajaribu kulikwepa korongo na kusababisha gari hilo kupinduka.


Ndani ya gari hilo kulikuwa kuna watu watatno ambao ni Snura na Minu pamoja na madancer wawili wa Snura pamoja na Dereva wa gari hilo lakini kwa bahati nzuri kila mtu ni mzima zaidi ya majeraha machache.


Mpenzi wa Snura ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu ajali hiyo:Jana mida ya saa nne usiku tulipata ajali mi na @snuramushi na ma-dancer wetu wawili pamoja na dereva.. Gari ilipinduka ila tunashkuru mungu tuko salama.. #WeGood


A post shared by 💣The CALYPTO💣 (@minu_calypto) on Aug 9, 2018 at 12:30pm PDT

The post Msanii Snura Mushi na Mpenzi Wake Wapata Ajali Ya Gari appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More