Msanii wa Filamu Shamsaford apost picha ikimuonyesha na majeraha usoni,maneno yake yaonyesha kupigwa na mume wake - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Msanii wa Filamu Shamsaford apost picha ikimuonyesha na majeraha usoni,maneno yake yaonyesha kupigwa na mume wake

Star wa Filamu Hapa Nchini Shamsaford ameamua kutoa yaliyo Moyoni kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram na kuelezea jinsi anakerwa na tabia za Wanaume ambao wanawanyanyasa Wake zao ambao walifunga nao Ndoa.Kauli hiyo ya Shamsa imeambatana na picha yake Ikimuonesha akiwa na alama usoni ya Kupigwa Pembeni ya Jicho la Kushoto na kuandika hivi ” wanawake ambao tuna mapenzi ya dhati ndo huwa tunaonewa sana.Wanawake ambao huwa tunaishi maisha ya uhalisia kutokana na mifuko ya wanaume zetu ndo tunaonewa na kuonekana washamba.Lakini wale wanawake wachunaji ndo huwa wanapewa kipaumbele na kuthaminiwa .Sielewi wanaume huwa wanataka nn kutoka kwa wanawake.Tunapigwa,tunasemwa vibaya,tunaonewa ,tunabeba mizigo mikubwa lakini mwisho wa siku bado unafuta machozi na kusema ALHAMDULILAH .Nyie wanaume huwa mnataka nini?🙌🙌 …”By Ally Juma.


The post Msanii wa Filamu Shamsaford apost picha ikimuonyesha na majeraha usoni,maneno yake yaonyesha kupigwa na mume wake appeared first on Bongo5.c... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More