Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda mwenye ukaribu zaidi na Bobi Wine auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda mwenye ukaribu zaidi na Bobi Wine auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana

Aliyewahi kuwa Msemaji wa jeshi la polisi mjini Buyende, Muhammad Kirumira ambaye pia amekuwa karibu na msanii wa muziki nchini humo, Bobi Wine ameuawa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani nyumbani kwake jana Jumamosi Septemba 8, 2018.


Kamanda Muhammad Kirumira (kushoto) akiwa na Bobi Wine

Kufuatia kifo hicho, Bobi Wine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyadondo ametuma salamu za rambi rambi kwa familia yake na kueleza ukaribu wake na Muhammad kupitia ukuarasa wake wa Twitter.


Am so saddened by the terrible news of the shooting of my good friend, and outspoken police officer, Muhammad Kirumira. Very sadly, that is the country we are living in. NO ONE IS SAFE. Our country is bleeding. This is very painful.Am so saddened by the terrible news of the shooting of my good friend, and outspoken police officer, Muhammad Kirumira. Very sadly, that is the country we are living in. NO ONE IS SAFE. Our country is bleeding. This is very painful. pic.twitter.com/8xucn7nYtl


— BOBI WINE (@HEBobiwine) September 9, 2018Tayari Jeshi la Polisi nchini Uganda limethibitisha taarifa hizo na limeahidi kuanza kufanya upelelezi kwa kina kuwapata wahalifu wa tukio hilo.The Uganda Police Force is greatly concerned with the assassination of ASP Muhammad Kirumira at Bulenga near his home at around 9:00pm. He was with a lady residents confirmed to be his wife. She too succumbed to bullet wounds and was pronounced dead on arrival at Rubaga Hospital


— Uganda Police Force (@PoliceUg) September 8, 2018Imeelezwa kuwa watu hao waliotekeleza shambulizi hilo walikuwa kwenye boda boda. Mwaka jana mwezi Marchi aliyekuwa msaidizi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kaweesi alishambuliwa na kuuawa katika eneo hilo hilo na watu wasiojulikana.


The post Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda mwenye ukaribu zaidi na Bobi Wine auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana appeared first on Bongo5.com.


Source: Bongo5Read More