MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA MKUU wa wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Assumpter Mshama amewaagiza watendaji wa vijiji na kata, kuhakikisha watoto wa wafugaji walio na umri wa kwenda shule, wanakwenda ili wapate haki ya elimu kama ilivyo kwa watoto wa jamii nyingine. 
Aidha ameeleza, wilaya inatarajia kuchukua sensa ya watoto wa wafugaji ili kupata idadi kamili ya watoto hao ambao hawaendi shule hadi sasa. 
Assumpter alitoa agizo hilo, wakati akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wafugaji na wakulima, kijiji cha Kwala, Kibaha Vijijini. 
Aliwataka ,wafugaji kuacha kuwatumikisha watoto wao kuchunga mifugo hasa ng'ombe badala ya kuwapeleka shule kupata elimu. 
"Watendaji nendeni mkahakikishe hakuna mtoto wa mfugaji anaefuga, hawa ndio Sokoine wa kesho, kwenye maziwa kuna akili, wanarubuniwa tuu, ila wafugaji watie akilini kwamba mtoto akizaliwa sio wako ni mali ya serikali "
"Haiwezekani wewe unaenjoy, mnakaa kujiolea wanawake 30, wakati watoto wako hawaendi shule, baadae hawa hawajui kama wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More