MSHAMBULIAJI MBRAZIL WA SIMBA SC, WILKER DA SILVA SASA YUKO FITI KUANZA KAZI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MSHAMBULIAJI MBRAZIL WA SIMBA SC, WILKER DA SILVA SASA YUKO FITI KUANZA KAZI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI Mbrazil, Wilker Henrique da Silva aliyekuwa majeruhi ameanza mazoezi Simba SC baada ya kupona maumivu yaliyokuwa yanamsumbua.
Taarifa ya SImba SC imesema kwama Silva mwenye umri wa miaka 23 amepona na sasa yupo tayari kuwatumikia na kuwapa furaha wapenzi wa timu hiyo.
Silva aliyesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu bingwa ya Tanzania Bara, Simba SC Julai mwaka huu akitokea klabu ya Bragantino inayocheza Ligi Daraja la Nne nchini kwao, Brazil hajaichezea timu hiyo hata mechi moja.
Kocha Mbelgiji wa Simba SC, Patrick Aussems akimuongoza mshambuliaji Mbrazil, Wilker Henrique da Silva mazoezi  

Wilker Henrique da Silva akimtoka kiungo Msudan, Sharaf Eldin Shiboub mazoezini Simba SC  

Lakini Wabrazil wengine wawili waliosajiliwa Simba SC msimu huu, mabeki Tairone Santos da Silva mwenye umri wa miaka 30 na Gerson Fraga Vieira mwenye umri wa miaka 26 anayeweza kucheza kama kiungo wa ulinzi pia wamekwishaanza kutumika.
Kwa upande wake, Tair... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More