MTANGAZAJI ISAAC GAMBA AFARIKI DUNIA NCHINI UJERUMAN, POLISI WAFANYA UCHUNGUZI WA KIFO CHAKE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTANGAZAJI ISAAC GAMBA AFARIKI DUNIA NCHINI UJERUMAN, POLISI WAFANYA UCHUNGUZI WA KIFO CHAKE


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MTANGAZAJI maarufu nchini Isaac Muyenjwa Gamba ambaye alikuwa akitangaza Idhaa ya Kiswahiliya DW ya Ujeruman amefariki dubia leo akiwa nyumbani kwake mjini Bonn nchini humo.

Taarifa ambazo Michuzi Blog imezipata kutoka kwa wafanyakazi wa DW ambao walikuwa wakifanya naye kazi kabla kifo kumkuta wanasema kwa sasa wanaendelea kufanya mawasiliano na familia yake ili kupata maelekezo.

Wamesema kifo cha Gamba kimewasikitisha na kimewashangaza kwani baada ya kuona hakufika ofisini juzi,jana na leo waliamua kutoa taarifa Polisi na walipoenda nyumbani kwake walivunja mlango na baada ya kuingia ndani walimkuta akiwa tayari amefariki dunia.

Wamesema baada ya Polisi wa nchini humo kuingia ndani waliukuta mwili wa Gamba kwenye kochi.Hivyo wakati wakifanya mawasiliano na familia pia wanasubiri uchunguzi wa Polisi kwanza na kisha waendelee na taratibu nyingine.

"Kwa upande wetu huku Ujeruman tunaendelea kuwasiliana na familia yake wakati tukiendelea kusubiri maj... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More