MTANGAZAJI ISACK GAMBA AFARIKI DUNIA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTANGAZAJI ISACK GAMBA AFARIKI DUNIA

Mtangazaji wa Idhaa ya Sauti ya Kiswahili (DW) ya Ujerumani, Isack Gamba amefariki dunia akiwa nchini humo.
Taarifa za awali za kifo cha mtangazaji huyo Mtanzania zinadai amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake akiwa amekaa kwenye kochi leo Alhamisi Oktoba 18, 2018.
Mmoja wa wafanyakazi mwenzake amesema kuwa jana Gamba hakuonekana kazini pamoja na juzi Jumanne jambo ambalo lilitia shaka.
“Hata leo Alhamisi, hakuonekana kazini asubuhi, ndipo tukaamua kwenda kutoa taarifa polisi, waliofika nyumbani kwake na kuvunja mlango wakamkuta Gamba ameshafariki dunia huku akiwa amekaa kwenye kochi.”
Amesema kuwa kwa sasa utaratibu unaofanyika ni kumpeleka kwenye uchunguzi na taarifa rasmi itafuata.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe.

Copyright 2007-2017 @KAJUNASON BLOG... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More