MTANGAZAJI WA CLOUDS SHAFII DAUDA AFIKISHWA KORTINI,APEWA DHAMANA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTANGAZAJI WA CLOUDS SHAFII DAUDA AFIKISHWA KORTINI,APEWA DHAMANANa Karama Kenyunko, blogu ya jamiiMTANGAZAJI wa Clouds na mmiliki wa mtandao wa Shafii Dauda,  Shafii Dauda Kajuna na Benedict Kadege  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.
Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka akisaidiana na mawakili Mutalemwa Kishenyi na Mwanaamina Kombakono wamewasomea washtakiwa shtaka lao mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina

Akiwasomea hati ya mashtaka Wakili Kombakono amedai kuwa  kati ya Juni 14 hadi Septemba mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shafii Dauda, washtakiwa kinyume cha sheria walitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Hata hivyo, baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa hao wamekana huku upande wa mashtaka ukidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hata hivyo Wakili Jebra Kambole anayewatetea washtakiwa hao aliomba Wateja wake hao wapewe dhamana... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More