MTANZANIA AMUANDIKIA SAMATTA KITABU. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTANZANIA AMUANDIKIA SAMATTA KITABU.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mtanzania Peter .W. Ching'ole ambaye ni mwanazuoni na mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii akiwa amehitimu shahada ya uzamili (Master's Degree) amemuandikia kitabu cha maisha ya soka ya mchezaji wa kimataifa anayekipiga nchini Ubelgiji Mbwana Samatta.
Ching'ole ameandika kitabu hicho kikiwa kinaelezewa maisha ya Samatta toka kuanza kwake kujihusisha na mpira mpaka hapa alipo sasa hivi akisaidiwa na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa mzazi wake Ally Samatta.
Kitabu hicho Kilichopewa jina la HUYU NDIYE MBWANA SAMATTA kimeweza kuonyesha Samatta akiwa na umri wa miezi tisa hadi ahapa alipo sasa hivi na kujua mwanzo wa maisha ya nyota huyo, wapi alipokulia ,familia yake, elimu aliyoipata na jinsi alivyoanza kucheza soka la mtaani mpaka soka la ushindani ambapo usajili wake kutoka African Lyon ulivyoweza kutikisa na kuzua utata mkubwa.
Ching'ole katika kitabu hicho ameelezea pia soka la kimataifa la nyota huyo, tuzo yake ya mchezajo bora wa Afrika, mafanikio ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More