MTENDAJI MKUU, MAHAKAMA YA TANZANIA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI YA UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTENDAJI MKUU, MAHAKAMA YA TANZANIA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI YA UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI

Na Festo Sanga, Mahakama ya Mkoa- Kigoma
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Husssein Kattanga amefanya ziara mkoani Kigoma na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu lililoanza kujengwa rasmi tarehe Oktoba 28, 2017 chini ya mkandarasi Masasi Construction Co Ltd. 
Ujenzi huo wa Jengo la Mahakama Kuu utasogeza huduma za Kimahakama karibu na wananchi wa Mkoa huo kwani wamekuwa wakisafiri kutoka Kigoma kwenda Tabora kufuata huduma za Mahakama Kuu.
Katika ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa Mahakama alipata fursa ya kutembelea mahakama ya Wilaya Kasulu na kukagua ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kasulu inayotegemewa kumalizika mwezi April 2019 chini ya Mkandarasi M/S Molad Tanzania LTD.
Ujenzi wa Mahakama mbalimbali nchini unalenga katika kusogeza huduma ya haki karibu zaidi na wananchi na vilevile ni utekelezaji dhahiri wa nguzo ya pili ya mpango mkakati wa Mahakama (2015/2016-2019/2020) ya upatikanaji wa haki kwa wakati.
Aidha ujenzi wa jingo hilo la Mahakama na unaotarajiwa kukamilika ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More