MTENDAJI MKUU TEMESA ATEMBELEA NA KUKAGUA KARAKANA MPYA IFAKARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTENDAJI MKUU TEMESA ATEMBELEA NA KUKAGUA KARAKANA MPYA IFAKARA

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto, Mhandisi Jairos Nkoroka (wa tatu kulia) pamoja na wafanyakazi wakikagua propella za vivuko vilivyohifadhiwa katika karakana ya mji wa Ifakara baada ya daraja la mto Kilombero kukamililika. Vivuko hivyo, MV.Kilombero I na II vitaanza kukarabatiwa na kuunganishwa hivi karibuni tayari kwa hatua ya kupelekwa katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma.  Mhandisi Jairos Nkoroka kushoto akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle mashine ya kugandamiza vipuri vya magari (press machine) wakati alipotembelea kukagua utendaji kazi wa karakana hiyo mpya ya TEMESA iliyoanza kutoa huduma mwezi Juni mwaka huu katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za karibu ikiwemo wilaya ya Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa zikitegemea kupata huduma Morogoro mjini. Mtendaji Mkuu wa W... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More