MTIBWA SUGAR ‘RONYA RONYA’, YAKAMILISHA MECHI TATU IKIPIGWA ZOTE KABLA YA KUIVAA SIMBA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTIBWA SUGAR ‘RONYA RONYA’, YAKAMILISHA MECHI TATU IKIPIGWA ZOTE KABLA YA KUIVAA SIMBA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro leo imekamilisha mechi tatu za kujiandaa na msimu mpya bila ushindi, ikipoteza zote baada ya leo pia kufungwa 1-0 na Reha FC ya Temeke Uwanja wa Bandari, Tandika katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa michuano ya Kombe la Reha Day.
Ikumbukwe, Mtibwa Sugar ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ilifungwa kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 na timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC  katika mchezo wa kwanza, hivyo kuangukia kwenye mechi ya kuwania nafasi ya tatu.
Awali ya hapo, Mtibwa Sugar inayofundishwa wachezaji wake wa zamani, kocha Zubery Katwila anayesaidiwa na Patrick Mwangata chini ya Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Mayanga ilifungwa 2-1 na Mbeya City Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Matokeo haya yanamaanisha Mtibwa Sugar hawako vizuri kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC Agosti 18 mwaka huu Uwanja... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More