MTIBWA SUGAR WAWASILI SALAMA MAHE TAYARI KWA MCHEZO WA MARUDIANO NA NORTHEN DYNAMO KESHO SHELISHELI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTIBWA SUGAR WAWASILI SALAMA MAHE TAYARI KWA MCHEZO WA MARUDIANO NA NORTHEN DYNAMO KESHO SHELISHELI

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM 
KIKOSI cha Mtibwa Sugar ya Morogoro kimewasili salama mjini Mahe, Shelisheli tayari kwa mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam na wenyeji, Northen Dynamo kesho Uwanja wa Linite huko Glacis.
Mtibwa Sugar iliondoka nchini jana ikipitia Dubai na baada ya saa zaidi ya nane iliwasili Mahe tayari kwa mchezo huo ambao itahitaji sare tu kusonga mbele baada ya ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam Jumanne iliyopita.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 11:30 kwa saa za Shelisheli na Saa 10:30 kwa saa za Afrika Mashariki Uwanja wa Linite mjini Glacis.

Mechi hiyo itachezeshwa na refa Eric Manirakiza atakayesaidiwa na washika vibendera, Hervé Kakunze na Ramadhani Nijimbere, wote wa Burundi.
Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza shujaa wa Mtibwa Sugar alikuwa ni mshambuliaji Jaffar Salum Kibaya aliyefunga mabao matatu, huku bao la nne likifungwa mtokea benchi Riffat Khamis Msuy... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More