MTIBWA SUGAR YAMTIA KITANZI MCHEZAJI BORA KOMBE LA TFF, ISMAIL AIDAN MHESA HADI 2021 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MTIBWA SUGAR YAMTIA KITANZI MCHEZAJI BORA KOMBE LA TFF, ISMAIL AIDAN MHESA HADI 2021

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa  Azam Sports Federation Cup (ASFC), Mtibwa Sugar wamefanikiwa kuingia mkataba mpya na kiungo wake mshambuliaji Ismail Aidan Mhesa.
Mhesa alikuwa anatumikia mwaka wake wa mwisho ambao ungemalizika mwishoni mwa msimu huu na sasa ameongeza miaka miwili hivyo Ismail Aidani Mhesa ataendelea kudumu Mtibwa Sugar hadi 2021.
Akizungumza na tovuti hii leo, Abubakar Swabr juu ya mkataba wa Mhesa amesema wameboresha mkataba wa awali na hivyo ataendelea kuitumikia Mtibwa hadi 2021.

Ismail Aidan Mhesa ataendelea kuitumikia Mtibwa Sugar hadi mwaka 2021

“Tumefikia makubaliano na Ismail Aidan Mhesa ya kuongeza miaka miwili na alikuwa anatumikia mwaka wake wa mwisho hivyo tumefikia makubaliano ataendelea kudumu Mtibwa Sugar hadi 2021, ni furaha kwetu kwa kwakuwa tumemuongeza mkataba mtu sahihi kutokana na kipaji kikubwa alichonacho” amesema Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabr.
Ismail Aidan Mhesa alijiunga na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar tangu 201... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More