Mtoto wa Rais mstaafu wa Afrika kusini Jacob Zuma, akumbwa na tuhuma za rushwa, azikana tuhuma hizo “Walitaka kuniua” – Video - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mtoto wa Rais mstaafu wa Afrika kusini Jacob Zuma, akumbwa na tuhuma za rushwa, azikana tuhuma hizo “Walitaka kuniua” – Video

Mtoto wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Duduzane Zuma amekataa tuhuma kuwa alitaka kumpa rushwa hiyo aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha.

Duduzane Zuma (35) alikana akiwa mbele ya Mahakama wakati akijibu tuhuma za kuwa kiunganishi cha mnyororo wa rushwa uliotengenezwa na Baba yake.Mcebisi Jonas aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha amesema kuwa Ajay Gupta kutoka familia ya wafanyabiashara wakubwa nchini humo alikuwepo katika kikao hicho kilichoandaliwa na Duduzane na kusema alimwonya asiongee tena juu ya mkutano huo. “Wangeweza kuniua,” alimwambia Zondo, na kuongeza kuwa “alitikiswa sana” baada ya mkutano.

Duduzane amekana kuwa katika kikao hicho hakukuwa na ahadi ya fedha wala Ajay Gupta hakuwepo eneo hilo.


“Hakuna ofa yoyote iliyotolewa,” Zuma aliambia tume ya uchunguzi iliotengwa na naibu jaji mkuu Raymond Zondo.


Baba yake Zuma, Jacob, alizungumzia uchunguzi huo mnamo Julai alieleza kwamba “ameshughulikiwa kama mtu anayeshtakiwa” kulingana na mawakili wake.


“Ni... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More