MUFTI TANZANIA: BAKWATA HAITAVUMILIA KUNYANYASWA NA KUVUNJIWA HESHIMA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MUFTI TANZANIA: BAKWATA HAITAVUMILIA KUNYANYASWA NA KUVUNJIWA HESHIMA

Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania halitavumilia tena kunyanyaswa, kuvunjiwa heshima au kuvunjiwa adabu na mtu yeyote.
Mufti wa Tanzania

Shehe Mkuu amesema, Bakwata haitaacha uislamu uchezewe na amewaomba mashehe, maimamu na maustaadhi waheshimu mamlaka na wawe watiifu kwa viongozi.
Amewataka Waislamu warudi kwenye mstari, wajenge mshikamano na amani, wajitambue, wabadilike, waache mazoea na kwamba, amewasamehe waliosema mabaya kuhusu Bakwata.
Ameomba Serikali ielewe kwamba, kwenye masuala ya Waislamu nchini wa kusikilizwa ni Bakwata na kwamba, baraza hilo linasema vitu sahihi kwa mujibu wa Katiba kwa kuwawakilisha Waislamu Tanzania.
“Haivumilii tena kama ilivyokuwa zamani, nikisema haivumilii tena kila mmoja atakuwa na tafsiri yake…hatuvumilii tena, lazima tuhakikishe kwamba Waislamu wanaelewa, na naomba Serikali inielewe wakati nazungumza mambo haya, mnielewe nazungumza kitu gani” amesema.
Ametoa mwito kwa Waislamu Tanzania wazidishe mshikamano, umoja, u... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More