Muhimbili kusuka upya mfumo wa kliniki - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Muhimbili kusuka upya mfumo wa kliniki

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umesema unaangalia jinsi ya kuboresha mfumo wa kliniki ili wagonjwa wahudumiwe kwa wakati baada ya kufika katika hospitali hiyo kupata huduma za matibabu.Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru wakati akizungumza na madaktari bingwa wa Muhimbili kuhusu namna bora kuboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo.Hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa nje 1,500 kwa siku. Pia, kuna wagonjwa 1,200 hadi 1,300 wamelazwa wodini wakati wote. Aidha wagonjwa wa nje walio wengi wanapenda kuja asubuhi hata kama kliniki zao zinaanza mchana.Prof. Museru amesema hatua hii ina lengo la kuboresha huduma katika kliniki hizo ni  kuondoa msongamano wakati mgonjwa au wagonjwa wakisubiri kuona madaktari bingwa wa hospitali hiyo.
“Wakuu wa idara kupitia kwa madaktari mtuletee mapendekezo ambayo tutaangalia jinsi ya kujenga mazingira bora ambayo wagonjwa watatumia muda mfupi kumuona daktari. Tunataka mgonjwa asikae m... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More