Muhimbili-Mloganzila yainyuka mabao 6 kwa nunge timu ya Albino United - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Muhimbili-Mloganzila yainyuka mabao 6 kwa nunge timu ya Albino United

Timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila (Mloganzila Sports Club) imeichapa mabao 6-0 timu ya Albino United ya Kibamba, mchezo uliyofanyika leo katika kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo chekundu jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo bao la kwanza lilifungwa dakika ya 18 kipindi cha kwanza na mchezaji machachari Jamal Msuya kutoka timu ya Mloganzila.Wafungaji wa mabao mengine kutoka timu hiyo ya Mloganzila Sports Club ni Ashirafu Katenda, Edger Mtitu na Adam Kingwande wakati magoli mawili yalifungwa na Goodluck Manji.
Katika mechi hiyo wachezaji wa Mloganzila walionekana kumiliki mchezo na kuhakikisha timu yao inaibuka na ushindi mnono.Hadi dakika tisini timu ya Albino United haikuweza kutikisa nyavu za wapinzani wao ambao ni Mloganzila Sports Club.
Awali kabla ya kuanza kwa mechi hiyo Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila Dkt. Mohamed Juma Mohamed amewapongeza wachezaji wote kwa kushiriki mchezo huo wa kira... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More