Muhimbili wahitimisha huduma za afya kwa njia ya mkoba katika Hospitali ya Rufaa Lindi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Muhimbili wahitimisha huduma za afya kwa njia ya mkoba katika Hospitali ya Rufaa Lindi

Watalaam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) ambao walikua wakitoa huduma za afya kwa njia ya mkoba katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi SOKOINE wamehitimisha huduma hiyo leo kwa kuwahudumia zaidi ya wagonjwa 1103 na kufanyia upasuaji wagonjwa 47.
Maeneo ambayo wataalam wa Muhimbili wamehudumia kwa kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Sokoine ni upasuaji, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho,watoto, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya dharura, Radiolojia pamoja na magonjwa ya ndani.

Mbali na kutoa huduma hizo lakini pia watalaam wa Muhimbili wamewajengea uwezo kiutendaji wataalam wa hospitali hiyo pamoja na kuleta mabadiliko ikiwemo kuelekezwa jinsi ya kanzisha idara na kuzisimamia ili kuleta ufanisi katika utoaji huduma.

Akizungumza katika kikao cha tathimini ya utoaji huduma, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija amesema kuanzishwa kwa idara mbalimbali kutaleta mabadiliko makubwa katika kutimiza majukumu yao kuanzia ngazi ya chin... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More