Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma

Na John Stephen, MusomaHospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeongeza siku saba zaidi kwa watalaam wake walioko Hospitali ya Rufaa Musoma ili kuhakikisha wanahudumia idadi ya wananchi wengi waliojitokeza kwa wingi kupata huduma katika kambi maalumu iliyoanza Oktoba 7, 2018 mkoani Mara.
Kambi hiyo ilitarajiwa kuisha leo Oktoba 12, 2018, lakini kutokana na hitaji kubwa la wananchi waliojitokeza kupata huduma, uongozi wa hospitali umeamua kuongeza siku hadi Ijumaa ijayo tarehe 19 Oktoba, 2018 ambapo watahitimisha na kurejea jijini Dar es  Salaam.
Hadi kufikia jana Alhamisi jumla ya wananchi  1210 walikuwa wamejiandikisha kupata huduma mbalimbali za matibabu kati hao   wananchi 1155 wameonwa na watalaamu  wa Muhimbili wale wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Musoma.
Kati ya hao, kinamama watano wamefanyiwa upasuaji, 36 wenye matatizo ya macho wamepatiwa huduma ya upasuaji, wagojwa wanane wamepatiwa huduma ya upasuaji wa mfumo wa mkojo, 14 upasuaji wa magonjwa mbalimbali (general surgery), 10 ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More