MUHIMBILI YAPOKEA MASHINE MPYA YA KISASA YA KUCHUNGUZA NA KUPIGA PICHA WAGONJWA WA MACHO. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MUHIMBILI YAPOKEA MASHINE MPYA YA KISASA YA KUCHUNGUZA NA KUPIGA PICHA WAGONJWA WA MACHO.

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv Dar es Salaam
Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia idara ya watoto imepokea Mashine mpya ya kisasa ya kuchunguza na kupiga picha kwa wagonjwa wa macho wanaofika hospitalini hapo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Rawlence Mseru amesema mashine hiyo yenye uwezo wa kupiga picha nyuma ya retina itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la wagonjwa kutoka hospitalini happy kwenda kufanya vipimo sehemu nyingine.
"Mashine hii ya kisasa imenunuliwa na kikundi Cha kwaya ya watoto kutoka kanisa kuu London uingereza ambalo watoto hao walichangishana na kununua mashine hii yenye thamani zaidi ya milioni 100"
Kwa upande wake Dr John Kisimbi Daktari bingwa wa magonjwa ya macho kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili idara ya watoto Amesema kuwa kwa Sasa mashine hiyo katika hospitali hiyo ni Moja tu tangu ile iliyonunuliwa miaka ya nyuma kuharibika kutokana na kukaa kwa muda mrefu.
Ametaja kuwa uwepo wa mashine hiyo... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More