Muhimbili yashirikiana na Mkemia Mkuu kutambua ndugu wa majeruhi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Muhimbili yashirikiana na Mkemia Mkuu kutambua ndugu wa majeruhi

Na Sophia Mtakasimba
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali wanaendesha zoezi la kuwapima vinasaba majeruhi ambao hawajitambui wa ajali ya moto iliyotokea Morogoro ili kubaini ndugu zao halisi.
Katika taarifa aliyoitoa katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa hospitalini hapo Bw.Aminiel Aligaesha alisema kuwa awali hospitali ilitoa wito wa ndugu kujitokeza kutambua majeruhi, lakini walijitokeza ndugu zaidi ya mmoja kwa majeruhi mmoja.
“Hii imeleta mkanganyiko hivyo tumeona tushirikiane na wenzetu wa Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili wachukue vinasaba vya wagonjwa na kulinganisha na ndugu waojitokeza ili kuhakikisha kwamba zoezi hili haliingii dosari,” alisema Bw.Aligaesha .
Kuhusu hali za majeruhi wa moto Bw. Aligaesha alisema kuwa kati ya majeruhi 46 waliopokelewa, 8 wamefariki dunia, 13 wapo katika wodi ya mahitaji maalumu na hawajitambui, 25 wanajitambua na wapo katika wodi za... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More