MUHIMBILI YAWASHUKURU WACHANGIA DAMU- ASANTENI SANA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MUHIMBILI YAWASHUKURU WACHANGIA DAMU- ASANTENI SANA

Muhimbili yawashukuru wachangia damu

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewaita na kuwashukuru watu waonajitolea kuchangia damu na mazao ya damu mara kwa mara ambayo imekuwa ikitumika kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji.

MNH imewaita wachangia damu na kuwashukuru ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya uchangiaji damu duniani ambayo hufanyika Juni 14, kila mwaka.

Akizungumza leo na wachangia damu kabla ya kuwakabidhi vyeti vya kutambua mchango wao, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa MNH, Dkt. Praxeda Ogweyo amewashukuru kwa kujitolea damu mara kwa mara kila wanapohitajika.

“Mwenyezi Mungu awabariki sana. Pia, tunaomba muwe mabalozi wetu kwa jamii nzima ili nao waige mfano wenu wa kujitolea damu ambayo inatumika kuokoa maisha ya watu wengine. Pia, napenda kuwashukuru wafanyakazi wa kitengo cha damu kwa kutoa huduma bila kuchoka. Bila jitihada zenu, tusingeweza kuwepo hapa siku hii muhimu,” amesema Dkt. Ogweyo.

Dkt. Ogweyo amesema mahitaji ya damu ni makubwa na kwamba uhitaji... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More