MultiChoice Tanzania yatangaza fursa kwa wadau wa filamu, yaja na program ya Talent Factory Portal - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MultiChoice Tanzania yatangaza fursa kwa wadau wa filamu, yaja na program ya Talent Factory Portal

MultiChoice Tanzania imetangaza fursa ya kipekee kwa wadau wa tasnia ya filamu Tanzania na barani Afrika kwa ujumla ijulikanayo kama MultiChoice Talent Factory Portal iliyodhamiria kuleta mapiduzi ya hali ya juu katika uaandaaji wa filamu zenye viwango vya kimataifa kutoka barani Afrika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano kutoka MultiChoice Tanzania Johnson Mshana alieleza kuwa programu hiyo ni muendelezo wa program maalum ya iliyodhamiria kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu barani Afrika. “MultiChoice Talent Factory ambayo ni progamu mama ilizinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka jana na imedhamiria kuleta mabadiliko chanya kwenye tasnia ya filamu hapa nyumbani Tanzania na Afrika kwa ujumla. Tulianza kwa kupeleka vijana wanne katika kambi maalum ya mafunzo ya uandaaji filamu katika akademia maalum kule Nairobi nchini Kenya, kisha mafunzo maalum kwa magwiji wa sauti yaliyofanyika mnamo mwezi Januari mwaka huu na hatimaye leo hii t... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More