Muna Akumbwa na Skendo Ya Kutelekeza Mtoto - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Muna Akumbwa na Skendo Ya Kutelekeza Mtoto

Msanii wa nyimbo za Injili Rose Alphonce Nungu maarufu kama Muna Love amejikuta katika skendo nzito ya kutelekeza mtoto wake wa kumzaa.


Global Publishers wanaripoti kuwa pamoja na Muna kunukuliwa akisema kwamba Patrick alikuwa mwanaye pekee, lakini nyuma yake kuna madai kuwa alizaa mtoto mmoja wa kiume (jina linahifadhiwa kimaadili) mwenye umri wa miaka 13.


Katika mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Ndugu yaka na Muna alimwaga ubuyu kuwa, kitendo cha Muna kutangaza kuhudumia watoto wa watu wengine huku akimuacha mtoto wa kumzaa akiwa analelewa na watu wengine, kinawakwaza ndugu walio wengi.Tunashangaa sana Muna huwa hamtambulishi kabisa mtoto wake mkubwa na nasikia alisema aliwahi kuzaa mtoto akafa wakati mtoto yupo hai na anatakiwa apate upendo kutoka kwa mama yake.


Kinachouma ni kwamba Muna sijui ataishi maisha ya kuigiza mpaka lini ilihali anawasaidia watoto wenye matatizo, hatukatai ni wajibu yeye kusaidia, lakini amwangalie na mtoto wake ambaye alimtoa katika tumbo lake. ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More