Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani

Dar es Salaam. Muogeleaji wa Tanzania, Natalia Ladha ametamba kufanya vyema katika mashindano ya kuogelea ya kutafuta tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya jimbo la Florida nchini Marekani yajulikanayo kwa jina la Florida Gold Coast Junior Olympic.
Natalia aliondoka nchini jana tayari kwa mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Martin County Juni 16 ambapo atajiunga na waogeleaji wa klabu ya Swimfast.
Muogeleaji huyo ambaye ni nyota kwa waogeleaji wa Tanzania wenye umri kati ya miaka tisa na 10, anashindana katika mashindano hayo makubwa matano Marekani kwa mara ya pili mfulilizo.
“Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na natarajia kufanya vyema kwa waogeleaji wenye umri kama wangu, nimejiandaa vyema katika nikiwa na makocha wangu wa klabu ya Taliss,” alisema Natalia.
Katika mashindano yam waka jana ya Miami, Natalia alishinda medali ya shaba kwa mita 50 na 100 kwa upande wa staili ya backstroke.
Natalia pia alitamba katika mashindano ya staili nyingine ambapo alitwaa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More