MUWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI AKABIDHI MIPIRA YA MAJI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MUWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI AKABIDHI MIPIRA YA MAJI.

Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar
MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amewaomba wananchi wa magomeni wandaras kuwa na mashirikiano na viongozi wao ili wanapopeleka huduma muhimu za maendeleo kwa jamii zipate ufumbuzi.
Hayo ameyasema huko Magomeni Wandaras wakati alipokuwa akikabidhi wananchi mipira ya maji katika shehia hiyo ikiwa anatimiza ahadi yake ili wananchi wa shehia hiyo waweze kupata huduma ya maji safi na salama kwa ukaribu na kupunguza masafa marefu yaliyokuwa yakiwakabili.
Amesema iwapo viongozi wa jimbo wanajitokeza kwa kuleta huduma za maendeleo inapaswa kuthamini na kuyafanyia kazi kwa moyo mmoja ili na wao waweze kufarijika zaidi na kuongeza kutatua changamoto nyengine zitazojitokeza .
Amesema wakati mliponichagua niliahidi kutatua changamoto na kuleta mambo ya maendeleo katika jimbo kati ya ahadi hizo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu miongoni mwa hayo ni maji safi na salama hii ikiwa ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More