Mvua zaacha balaa Dar - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mvua zaacha balaa Dar

Kila majira ya mvua yafikapo basi majanga kama haya kwa mji wa Dar es salaam ni lazima uyaone, maji kujaa huku na kule, mitaro ya maji kujaa, barabara kufungwa na hata vifo pia hutokea. Siku chache zilizopita barabara mbalimbali jijini humu ziliripotiwa kufungwa kufuatia kujaa kwa maji mengi barabarani.


Eneo hili la barabara ya jangwani kwa sasa lipo kwenye ukarabati unaohusisha kuondoa matope na michanga iliyoziba barabara pamoja na takataka nyingi zilizoletwa na maji ya mvua. Lakini pia wananchi wa maeneo haya ya karibu na daraja hili la jangwani wamelalamikia miundo mbinu mibovu katika eneo hilo kuwa ndio chanzo cha maji kujaa, na kuongezea kuwa wanapata ugumu mwingi pindi maji yakijaa na pale ambapo huduma za usafiri zikisitishwa.  Tweet


Source: Kwanza TVRead More