Mvutano kati ya Anthony Joshua na Andy Ruiz, Ulipelekea pambano la marudiano kupangwa Saudia Arabia - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mvutano kati ya Anthony Joshua na Andy Ruiz, Ulipelekea pambano la marudiano kupangwa Saudia Arabia

Pambano la marudiano kati ya Andy Ruiz Jr na Anthony Joshua litafanyika mwezi Disemba nchini Saudi Arabia, promota wa Joshua Eddie Hearn amethibitisha. Kumekuwa na tetesi kuwa Ruiz Jr hayupo tayari kwa pambano hilo, lakini Hearn amesema kuwa mabondia wote wawili wameshaini kucheza mpambano huo Disemba 7 mwaka huu. Ruiz aliushangaza ulimwengu wa masumbwi kwa kumchakaza Joshua mwezi Juni na kutawazwa kuwa bingwa wa dunia.Bingwa huyo mpaka sasa hajawaarifu chochote mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na mpambano huo wa marejeano toka ulipotangazwa siku ya Ijumaa.


Mkufunzi wake, Manny Robles amesema “kuna sababu inayommfanya” Ruiz kukaa kimya.


“Mabondia wote wawili wameshatia saini. Vyombo vya usimamizi (wa ndondi) vimeshaarifiwa,” amesisitiza Hearn.


Katika mkutano na wanahabari, ambao hata hivyo si Joshua wala Ruiz ambaye alihudhuria, Hearn alitangaza kuwa mpambano huo utafanyika katika uwanja wa wazi katika kitongozji cha Diriyah, nje kidogo ya jiji la Riyadh.


... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More