Mwanafunzi anaswa na polisi baada ya kumkaba mama yake mzazi na kumpora - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwanafunzi anaswa na polisi baada ya kumkaba mama yake mzazi na kumpora

Jeshi la Polisi jijini Dodoma linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari ya Itega, Mohamed Ramadhani (18) kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu ikiwa ni pamoja na kumkaba mama yake mzazi.


Mwanafunzi huyo anatuhumiwa kujiunga na kikundi cha uhalifu cha Kamchape ambacho kinajihusisha na ukabaji na uvunjaji katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa jiji la Dodoma, Gilles Muroto alisema kuwa kijana huyo amekuwa akijishughulisha na uhalifu ambapo kwa siku za hivi karibuni aliwahi kukiri kumkaba mama yake mzazi lakini mama huyo hakujua kuwa aliyemkaba ni mwanaye.

“Huyu kijana alijua kuwa aliyemkaba na kumpora ni mama yake mzazi, hivyo alivyogundua  aliyempora ni mama yake alichofanya ni kumwachia mkoba aliompora na kutokomea kusikojulikana bila yule mama kufahamu, kuwa aliyemkaba ni mwanaye wa kumzaa”, alisema Muroto

Aidha, Kamanda Muroto alisema baada ya tukio hilo kijana huyo aliachiwa lakini ali... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More