Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet

 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, Ibrahim Pius Mbwilo (28) ameshinda Sh 239,417,800 kupitia mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na kampuni ya M-Bet.

Mbwilo ambaye anasoma shahada ya Utawala wa Biashara (Business Administration) akiwa mwaka wa pili, alibashiri kiusahihi mechi 12 za ligi mbalimbali za ulaya. Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi alisema kuwa Mbwilo ambaye ni shabiki wa timu ya Simba na Chelsea ya Uingereza, amekuwa mshindi wa pili kupata fedha nyingi zaidi tokea kuanzishwa kwa droo ya Perfect 12. Mshindi wa kwanza alipata Sh 280 millioni.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwasaidia watanzania kubadili maisha yao kwa kutumia Sh1,000 tu. “Nawaomba Watanzania kuendelea kubashiri kwa kutumia michezo yetu,kuna nafasi kubwa ya kushinda na mpaka sasa tumepata jumla ya washindi 10 ambao wamefaidika na droo yao,” alisema Mushi.

Alisema kuwa Serikali imepata Sh 47 millioni kutokana na kodi kutokana na ushindi huo wa Mbwilo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More