MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI

Na Yeremias Ngerangera, NamtumboMwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo  kikuu cha Dodoma ( UDOM)kitivo cha elimu amekwama nauli ya kufika chuoni  baada ya wazazi  wake kutamka bayana kuwa hawana uwezo hata  ya kupata nauli ya kumsafirisha  binti yao kufika chuoni .Bahati  Njete (21) mkazi wa Minazini wilayani Namtumbo amechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma  huku  wazazi wake hawana  uwezo  hata wa kumpatia  nauli ya kufika  chuoni  ili  akaendelee  na masoma yake.Akiongea  na Ofisa ustawi wa jamii wilaya ya Namtumbo Irene Kitula ofisini kwake  Bahati alisema  wazazi wake wanahali ngumu za kimaisha na mafanikio aliyoyapata ni kutokana na misaada ya wasamaria wema  ambao walijitolea kwa hali na mali kumsaidia toka kidato cha kwanza  hadi cha sita.Aidha  Bahati alidai kumaliza elimu ya sekondari katika sekondari ya kata Narwi  iliyopo wilayani Namtumbo na kisha kuchaguliwa kuendelea na masomo kidato cha sita katika shule ya sekondari ya  Igowole  iliyopo mko... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More