Mwanafunzi wa kidato cha nne ajiua kwa kujipiga risasi - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwanafunzi wa kidato cha nne ajiua kwa kujipiga risasi

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Arusha Meru, Faisal Salimu (19) amejiua kwa kujipiga risasi.


Mwanafunzi huyo amejipiga risasi kwa kutumia bunduki ya baba yake Salimu Ibrahim (59), aina ya Rifle Winchester akiwa amejifungia chumbani kwake katika nyumba ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), eneo la Soko Kuu jijini Arusha.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shani, amesema katika tukio hilo lilitokea Jumapili Agosti 18, 2019 saa 11 alfajiri, ambapo mwanafunzi huyo alijipiga risasi katika paji la uso.


Uchunguzi wa awali umebaini mwanafunzi huyo alikuwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo, kutokana na kushutumiwa kuwa anatumia dawa za kulevya.


“Tumeanza uchunguzi wa tukio hili na silaha hii kama ilikuwa inamilikiwa kihalali. Hatua za kisheria zitachukuliwa ikibainika kama silaha haikuhifadhiwa vizuri,” amesema Shana.Tweet... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More