Mwanamke afunga ndoa na mti ili kuunusuri usikatwe, fahamu zaidi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwanamke afunga ndoa na mti ili kuunusuri usikatwe, fahamu zaidi

Mwanamke mmoja kutoka nchini Uingereza aitwaye Kate Cunningham, ameamua kuishangaza jamii kwa uamuzi wake wa kufunga ndoa na mti. Cunningham ni mkazi wa Mjini Merseyside, Uingereza na harusi yake ilifungwa katika moja ya kumbi maarufu nchini humo, Merseyside Park.Si kwamba hajawaona wanaume, bali ni kwa sababu ya kufanya kampeni za kupinga ujenzi wa barabara, ambao kwa namna yoyote ile mti huo mkubwa na mingine iliyoko katika eneo la Rimrose Valley Park ingelazimika kukatwa.


“Nimekuwa nikiingia mitaani na maelfu ya watu kupinga uharibifu wa miti, lakini sioni hiyo ikiwa na nguvu zaidi kuwaamsha watu,” anasema Cunningham.


Wakazi wa Rimrose Valley Park, hawataki kuona eneo hilo likikatwa miti na kisha ipite barabara kwa kile wanachodai kuwa ni kwa usalama wa afya zao.


“Hii inanigusa moja kwa moja. Mama yangu alifariki kwa pumu na mimi nasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu… kuharibu eneo hili na kisha kuweka barabara haiingii akilini na ni hatari wa afya zetu,” anasisitiza.


Si tu k... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More