MWANAMKE APAMBANA NA JAMBAZI MWENYE SILAHA AKIMUOKOA MUMEWE, - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWANAMKE APAMBANA NA JAMBAZI MWENYE SILAHA AKIMUOKOA MUMEWE,

Na Felix Mwagara, (MOHA) MARA. 
Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Kata ya Nyamihyolo, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Busimba Malegesi amemuokoa mumewe asiuawe na jambazi mwenye silaha ambaye alivamia katika nyumba yao na kuanza kumshambulia mwanaume huyo kwa kumkatakata mapanga mwili mzima.

Busimba alimrukia jambazi huyo kiunoni na kumuangusha chini na kufanikiwa kumnyang’anya panga pamoja na tochi ambazo alikua nayo wakati anamshambulia mumewe aitwaye Samson Malegesi (62).

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 7:30 usiku wa kuamkia Ijumaa wakati familia hiyo ikiwa imelala ndipo jambazi huyo alivunja mlango na kuingia moja kwa moja chumbani kwa wanandoa hao na kuwasha tochi kumsaka Malegesi na baada ya kufanikiwa kumuona alianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga kichwani, mikononi, kwenye mbavu na kusababisha damu nyingi kumwagika.

Wakati jambazi hilo akiendelea kumshambulia Malegesi, mkewe alikua naye anapambana kwa kumzuia asimshambulie mumewe, lakini jambazi hilo lil... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More