Mwanamke wa kwanza kuchezesha michuano ya kimataifa ya wanaume barani Afrika atokea Tanzania - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwanamke wa kwanza kuchezesha michuano ya kimataifa ya wanaume barani Afrika atokea Tanzania

Mwamuzi Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuwa mwamuzi wa michuano ya vijana ya wanaume wenye umri wa chini ya miaka 17 inayofanyika hapa nchini.


Rukyaa ndiye mwanamke pekee atakayepuliza kipenga katika michuano hiyo.


Rukyaa pia aliwahi kuchezesha michuano ya AFCON ya wanawake mwaka jana huenda akapata fursa ya kutangaza zaidi jina lake kwenye michuano ya kombe la dunia la wanawake kule nchini Ufaransa.


Rukyaa ataweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha michuano ya kimataifa ya wanaume barani Africa.Jonesia ndiye mwanamke pekee atakayeshika kipenga kama mwamuzi wa kati. Wanawake wengine ni pamoja Mary Njoroge (Kenya) & Lidwine Rakotozafinoro (Madagascar) ambao wao watakuwa waamuzi wa pembeni.


CAF imeteua jumla ya waamuzi 29 ambao watasimamia sheria za FIFA katika michuano hiyo inayotatajia kutimua vumbi nchini haoa.


Waamuzi wote watakwenda kufanya semina kule Casablanca, Morocco kuanzia 31 March hadi kufikia 4 April 2019.


Hata hivyo Jonesia pia anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke wa ... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More