Mwanza, Songwe kucheza nusu fainali kesho UMISSETA Soka wavulana - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwanza, Songwe kucheza nusu fainali kesho UMISSETA Soka wavulana

Na Mathew Kwembe, MtwaraMichuano ya UMISSETA inayoendelea mjini Mtwara imefikia hatua ya nusu fainali kwa upande wa soka wavulana ambapo katika michezo iliyomalizika leo jioni, timu za soka wavulana kutoka mikoa ya Lindi, Ruvuma, Mwanza na Songwe zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuwalaza wapinzani wao akiwemo bingwa mtetezi Tanga ambayo ilitolewa na Lindi.Kwa matokeo hayo timu ya soka wavulana kutoka mkoa wa Lindi itakutana na Ruvuma kwenye nusu fainali ya kwanza inayotarajiwa kucheza kesho saa nane mchana na kufuatiwa na nusu fainali ya pili itakayowakutanisha vigogo Mwanza watakaochuana na timu ngumu ya Songwe.Timu ya kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ilikuwa ni timu machachari ya kutoka  mkoa wa Lindi ambayo iliitoa timu ya mkoa wa Tanga kwa penati 3 kwa 1 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana baada ya dakika tisini za mchezo.Pambano lingine la robo fainali lilizihusisha timu za kutoka mikoa Ruvuma na Kilimanjaro ambapo timu ya soka ya mkoa wa Ruvuma ambayo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More