MWANZA WAZINDUA MSIMU WA KILIMO CHA PAMBA KWA KUGAWA MBEGU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWANZA WAZINDUA MSIMU WA KILIMO CHA PAMBA KWA KUGAWA MBEGU

NA BALTAZAR MASHAKA MISUNGWI
WANANCHI wa vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wametakiwa kulima kilimo chenye tija kitakachowanufaisha kiuchumi na kuondokana na umasikini.
Rai hiyo ilitolewa jana katika Kijiji cha Seeke wilayani Misungwi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati akizindua msimu mpya wa kilimo cha pamba kwa kugawa mbegu za zao hilo pamoja na kamba za vipimo vya kupandia kitaalamu.Alisema wakulima walime kilimo cha kisasa cha kibiashara, wazingatie masharti na kanuni kumi bora za kilimo, wakifanya hivyo wataongeza uzalishaji na kupata maendeleo ya kiuchumi na kipato.
Mongela alisema kwa kuwa serikali imewaletea mbegu kwa wakati wajitume na kulima kwa bidii kwani bila kujibidisha itawawia vigumu kupata mavuno mengi na kuonya wanaume kuacha tabia ya kukaa kwenye vijiwe vya kahawa badala yake wajikite kwenye kilimo.Aliigiza Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuhakikisha inasambaza kwa wakati dawa za viuadudu (viautilifu), vikipungua taarifa itolewe mapema na kuwataka maofis... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More