MWASELELA AWASAIDIA WAJANE USHARIKA WA KKKT FOREST MBEYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWASELELA AWASAIDIA WAJANE USHARIKA WA KKKT FOREST MBEYA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Mbeya
Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela ametoa msaada kwa wajane wawili katika kanisa la KKKT Forest Mkoani Mbeya .


Mwaselela ambaye alipata nafasi ya kuzungumza na wanakwaya wa kwaya ya Safina ya kanisa hilo, ambapo aliomba apewe wajane wawili Ili aweze kuwapa mitaji ya kujikwamua kimaisha.


“Mimi ni Mtoto wa Mama ntilie ambaye nimefanikiwa leo hivyo niwaambie wazi, Mama yangu alikuwa anauza Supu ili mimi nisome, hivyo nina kila sababu  ya kuwasaidia watu mbalimbali wasiojiweza wakiwemp wajane,binafsi naona fahari kila ninapofika mahali  angalau niweze kuwagusa wanawake wawili” alisema Mwaselela.


Mwaselela amesema kuwa mbali ya kuwa mtoto wa Mama Ntilie, walitokea watu wakainuka wakanisomesha na wengine sasa ni wabunge na wamepata kushika nafasi za juu serikalini.


Amesema kuwa ni vyema watu wakajifunza kutoa na kusaidia wengine, kwani kwa kufanya hivyo Mungu hugusa pale walipotoa na kuwabariki kwa kila hatua wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More