MWENGE WA UHURU UNATARAJIA KUPITIA MIRADI 67 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BIL.162.440 MKOANI PWANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWENGE WA UHURU UNATARAJIA KUPITIA MIRADI 67 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BIL.162.440 MKOANI PWANI

NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amepokea mwenge wa uhuru ,ukitokea jijini Dar es salaam ,ambapo ukiwa mkoani hapo unatarajiwa kupitia miradi ya maendeleo 67 yenye thamani ya sh.bilioni 162.440.8 .
Kati ya miradi hiyo ,16 itawekwa mawe ya msingi ,miradi 13 itazinduliwa ,nane itafunguliwa na 21 itakaguliwa.Akikabidhiwa mwenge huo ,wilayani Mkuranga Ndikilo alisema ,mwenge wa uhuru ukiwa mkoani humo, pia utapitia wilaya 7 na halmashauri 9#.
Alisema mwenge wa uhuru utapokea taarifa ya miradi 9 katika maeneo mbalimbali ya mkoa na wamehakikisha miradi yote itakuwa na thamani ya fedha ili wasiangukie kwenye mtego ambao uliwakumba mkoa wa Dar es salaam.
Alieleza ,miradi hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano baina ya wananchi,serikali kuu,halmashauri na wahisani wa kitaifa na kimataifa." Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’
"Katika kutekeleza ujumbe huo tumejipanga kutekeleza kwa v... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More