Mwenye kidonda cha ajabu aanza matibabu Muhimbili - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwenye kidonda cha ajabu aanza matibabu Muhimbili

Hatimaye Mariam Rajab (25), mkazi wa Singida anayesumbuliwa na kidonda mgongoni, amepokewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.


Mariam ambaye video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu, amewasili hospitalini hapo saa sita usiku wa kuamkia leo Aprili 18.


Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, John Steven amesema Mariam amepokelewa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura.


“Mgonjwa tumempokea katika Idara ya Dharura, ambapo amelazwa huku akiendelea kufanyiwa vipimo vya awali ili aweze kuonana na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya kupatiwa matatibu zaidi” amesema Steven.


Amesema Mariam ameletwa na gari la wagonjwa (Ambulance) kutoka Singida ambapo safari yake ilianza jana saa 8:00 mchana.


Katika ujumbe wa video ulikuwa ukisambaa ulimuonesha Mariamu akiomba msaada wa kupatiwa matibabu ya kidonda kinachomsumbua.


“Mimi naitwa Mariam Rajabu naishi katika Mkoa wa Singida, Mtaa wa Mnung’una naishi katika fam... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More