MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA DKT MNDOLWA KUUPATIA UFUMBUZI MGOGORO WA MACHIMBO YA DHAHABU MKOANI GEITA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA DKT MNDOLWA KUUPATIA UFUMBUZI MGOGORO WA MACHIMBO YA DHAHABU MKOANI GEITA

Na Bashir Nkoromo, Geita.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuupatia ufumbuzi mgogoro wa machimbo ya dhahabu wa Lwamgasa mkoani Geita uliopo kati ya Jumuuya ya Wazazi mkoa wa Geita na Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza.

Mgogoro huo umeibuka tangu Geita ilipomegwa kuwa mkoa, na hivyo leseni ya machimbo hayo yaliyopo Geita huhodhiwa na Jumuiya Wazazi Mwanza huku machimbo yenyewe yakiwa kwenye mkoa wa Geita.

Mvutano wa umiliki wa machimbo hayo umekuja kutokana na Jumuuya ya Wazazi Geita kuona kuwa ni rasilimali yake lakini haipati chochote badala yake wanaofaidika nayo ni Mwanza. "Ninayo majembe (viongozi) ambao nikikaa nao tutaumaliza mgogoro huu, na hii ni Geita isiwasumbue sana hasa mkizingatia kuwa mali za jumuia ni mali za Chama". alisema Dk. Mndolwa.

Dk. Mndolwa ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha ndani na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Geita na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya za Chama kutoka wilaya za mkoa huo alisema, ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More