MWENYEKITI MPYA KAMATI BARAZA LA MAWAZIRI SADC PROFESA KABUDI ATAJA VITAKAVYOPEWA KIPAUMBELE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWENYEKITI MPYA KAMATI BARAZA LA MAWAZIRI SADC PROFESA KABUDI ATAJA VITAKAVYOPEWA KIPAUMBELE

Na Said Mwishehe,Michuzi Blog
MWENYEKITI mpya wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)Profesa Palamagamba Kabudi amesema kwamba nchi za Jumuiya hiyo zinapasaa kutumia sekta ya viwanda katika kuleta maendeleo na kuondoa umasikini.
Profesa Kabudi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,.ameyasema hayo leo Agosti 13,2019 baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo ya uenyekiti wa kamati ya baraza la mawaziri kwa nchi SADC . Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Netumbo Ndaitwah ambaye ni Naibu Waziri Mkuu wa Namibia.
Hivyo baada Waziri Kabudi kukabidhiwa nafasi hiyo pamoja na mambo mengine amesema nchi za SADC zinapaswa kufikia maendeleo kwa kasi, hivyo sekta ya viwanda ni njia muhimu kufikia lengo hilo na kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake atakikisha sekta ya viwanda inapaswa kipaumbele.
"Nitahakikisha nashirikiana na wenzangu katika kamati na viongozi wa nchi kuchochea ua... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More