Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya kusini amewataka Viongozi wa Majimbo kusikiliza kero za Vijana ili kuweza kuzipatia ufumbuzi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya kusini amewataka Viongozi wa Majimbo kusikiliza kero za Vijana ili kuweza kuzipatia ufumbuzi

Na Takdir Ali-Maelezo ZanzibarMWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini Abdul-aziz Hamad Ibrahim amewataka Viongozi wa Majimbo kusikiliza kero za Vijana ili kuweza  kuzipatia ufumbuzi.
Amesema vijana wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo hivyo iwapo Viongozi wanapita na kuwatatulia matatizo yanayowakabili wataweza kuongeza juhudi za kukipatia ushindi chama cha Mapinduzi ifikapo 2020.
Ameyasema hayo huko Tawi la CCM Kizimkazi Dimbani alipokuwa akizungumza na Vijana wa Tawi la Mpendae juu katika ziara ya kubadilishana mawazo na Vijana wa Tawi la CCM Kizimkazi Dimbani Wilaya ya Kusini.
Ameeleza kuwa Vijana wana matatizo mengi ikiwemo Ajira na elimu lakini baadhi ya Viongozi hawasaidii kitu chochote cha kuweza kujiendesha maisha  jambo ambalo linawavunja moyo na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
“Matatizo ya vijana ndani ya nchi  ni mengi ikiwemo ukosefu wa ajira hivyo viongozi wawasaidie vijana hao kwa kuwapa mitajiili waweze kujiendeleza katik maisha yao”. Alisema Mwenyekit... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More