MWENYEKITI WA UCHAGUZI TFF AWAONYA WANA YANGA WANAOTAKA KUTIBUA UCHAGUZI WATAKIONA CHA MOTO NA WATAJUTA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MWENYEKITI WA UCHAGUZI TFF AWAONYA WANA YANGA WANAOTAKA KUTIBUA UCHAGUZI WATAKIONA CHA MOTO NA WATAJUTA

Na Mwandishi Wetu, DODOMA
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewaonya vikali viongozi na mashabiki wa klabu ya Yanga wanaopanga kuvuruga mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo.
Yanga wanatarajiwa kufanya uchaguzi wake Januari 13, mwakani kwa ajili ya kuziba nafasi zilizokuwa wazi.
Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela, alisema TFF haitowavumilia wote watakaothubutu kuvuruga mchakato huo.
Mchungahela alisema kuwa wamebaini kwamba  kuna mkakati wa baadhi ya viongozi wa kamati ya utendaji na mashabiki wa kutaka  kuitisha mkutano kesho  wenye lengo la kupinga uchaguzi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela amesema TFF haitowavumilia  wanataka kuvuruga uchaguzi wa Yanga

“Taarifa zao tunazo, kwamba wanataka kuitisha kikao cha kupinga uchaguzi, hivyo sisi kama TFF tunawaonya wasithubutu, kwani tutawashughulikia kwa kutaka kuharibu mchakato huo na  pia yeyote yule anayetaka uongozi asipite mlango ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More